Friday, 21 March 2025

TRA: Vituo na Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili TRA Updates

  AjiraLeo Tanzania       Friday, 21 March 2025
WARNING
Beware of Job Scammers!
Please Never Pay Money To Get A Job!
TRA: Vituo na Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili TRA
TRA: Vituo na Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili TRA Updates

💥MASWALI YA USAILI TRA+OTHER UPDATES. CLICK HERE!💥

💥UNASUBIRI NINI? FOLLOW US ON INSTAGRAM. CLICK HERE!💥

Ajira Mpya TRA2025 - New Government Jobs at TRA 2025
TRA: Vituo na Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili TRA Updates
TRA: Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Mamlaka ya Mapato Tanzania Kutoka KeshoMkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Moshi Jonathan Kabengwe amesema majina ya waombaji wa ajira 1,596 za TRA zilizotangazwa hivi karibuni yatatangazwa rasmi Machi 22.2025 kupitia tovuti ya tra.go.tz na hapa www.ajiraleo.com kwa ajili ya usaili wa kuandika utakaofanyika Machi 29 na 30 mwaka huu kwenye vituo 9.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam leo tarehe 21.03.2025 Bw. Kabengwe amesema kati ya waombaji 135,027 waliotuma maombi ya nafasi za ajira, waombaji 112,952 wamekidhi vigezo na kuitwa kwenye usaili wa kuandika.
Amesema kila muombaji atatumiwa taarifa ya kuitwa kwenye usaili katika barua pepe yake aliyoiambatanisha kwenye maombi ya kazi na kuwa waombaji wenye mahitaji maalum wamewekewa utaratibu maalum ambao utawasaidia kufanya usaili bila usumbufu.

Vituo vya Usaili TRA kwa Watakaoitwa kwenye Interview Mamlaka ya Mapato TanzaniaLeo

Bw. Kabengwe amesema usaili huo utafanyika kwenye Mikoa 8 na Zanzibar ambayo ni:
1. Dar es Salaam ambayo itahusisha waombaji kutoka Dar es Salaam na
Pwani.

2. Zanzibar ambayo itahusisha waombaji kutoka Unguja na Pemba

3. Arusha ambayo itahusisha waombaji kutoka Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Tanga

4. Dodoma ambayo itahusisha waombaji kutoka Morogoro, Dodoma, Singida, Iringa na Tabora

5. Mtwara ambayo itahusisha waombaji kutoka Mtwara, Lindi na Ruvuma

6. Mbeya ambayo itahusisha waombaji kutoka Mbeya, Songwe na Rukwa

7. Mwanza ambayo itahusisha waombaji kutoka Mwanza, Shinyanga, Mara na Simiyu

8. Kagera ambayo itahusisha waombaji kutoka Kagera na Geita na

9. Kigoma ambayo itahusisha waombaji kutoka Kigoma na Katavi.
Endela kurembelea page hii ili uwe wa kwanza kuona majina punde tu yatakapotoka mdau!
logoblog

Thanks for reading TRA: Vituo na Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili TRA Updates

Previous
« Prev Post

No comments:

Post a Comment