Monday, 28 October 2024

YANGA WAKIKAZA HAPA WATAMPOTEZA MAZIMA SIMBA CAF

  AjiraLeo Tanzania       Monday, 28 October 2024
WARNING
Beware of Job Scammers!
Please Never Pay Money To Get A Job!
YANGA WAKIKAZA HAPA WATAMPOTEZA MAZIMA SIMBA CAF
Baada ya timu za Yanga na Simba kufanikiwa kufuzu makundi ya CAF kama nchi (Tanzania) tumeongeza pointi 7.5 (Yanga pointi 5, Simba Pointi 2.5) na kufikisha pointi 60 nafasi ya sita kwenye Association Ranking na tumezidiwa na mataifa matano (Misri-135.5, Morocco-104.5, Algeria-95, Afrika Kusini-83.5, Tunisia-72.5).

YANGA WAKIKAZA HAPA WATAMPOTEZA MAZIMA SIMBA CAF

Nafasi ya 7 wapo DR Congo na Angola wakiwa na pointi 45 kila mmoja huku anayeshika nafasi ya 13 ana pointi 18.5 hivyo tuna misimu 2 hadi 3 mbele ya kupeleka timu 4 kwenye mashindano ya CAF (2 klabu bingwa Afrika na 2 kombe la shirikisho) hata timu zetu hazitafanya vizuri kwa kufika makundi ya kombe la shirikisho au klabu bingwa.
YANGA WAKIKAZA HAPA WATAMPOTEZA MAZIMA SIMBA CAF
Kwenye Club Ranking mpaka sasa timu ya Simba ipo nafasi ya saba ikiwa na pointi 30.5 na Yanga ipo nafasi ya 11 ikiwa na pointi 29 kama nchi tuna pointi 60 (Simba 30.5, Yanga 29, Namungo 0.5) wanaongoza ni 1-Ahly-63, 2-Esperance-47, 3-Mamelodi-42, 4-Wydad-39, 5-Zamalek-34.5, 6-Belouizadad-31, 7-Mazembe & Simba 30.5, 9-Berkane & USM Alger-29.5, 11-Yanga 29.

Kwenye hizo timu 11 za juu timu moja tu ya Wydad ndio haipo kwenye mashindano zingine zote zipo kwenye hatua ya makundi ikiwa Ahly, Esperance, Mamelodi, Belouizdad, Mazembe na Yanga zipo makundi ya klabu bingwa Afrika huku Zamalek, Simba, Berkane na USM Alger zipo makundi ya kombe la shirikisho.

Timu ambazo zipo makundi zinaweza kuongeza pointi kulingana na performance yao kwa msimu huu kulingana na nafasi ambayo wataishia. Pointi huwa zinapatikana kama ifuatavyo kila pointi unayoipata kila msimu kulingana na nafasi uliyoishia unazidisha na coefficient code ya msimu husika
Zifuatavyo ni code kwa msimu mitano inayopigiwa hesabu kutafuta pointi 2024/25=5 2023/24=4 2022/23=3 2021/22=2 2020/21=1

Pointi zinapatikana kama ifuatavyo >Kwenye klabu bingwa Afrika (CAF Champion League) Bingwa=6 Mshindi wa pili = 5 Nusu fainali =4 Robo fainali =3 Nafasi 3 kwenye kundi = 2 Nafasi ya 4 kwenye kundi =1
READ ALSO:
Kwenye kombe la shirikisho (CAF Confederation Cup) Bingwa=5 Mshindi wa pili = 4 Nusu fainali =3 Robo fainali =2 Nafasi 3 kwenye kundi = 1 Nafasi ya 4 kwenye kundi =0.5
Pointi zinapatikana kwa kuchukua pointi ya nafasi uliyoishia unazidisha na coefficient code ya msimu husika

Simba ina pointi 30.5 ikiwa 2024/25 Makundi (Shirikisho) 0.5×5 = 2.5 2023/24 Robo (Klabu Bingwa) 3×4 = 12 2022/23 Robo (Klabu Bingwa) 3×3 = 9 2021/22 Robo (Shirikisho) 2×2= 4 2020/21 Robo (Klabu Bingwa) 3×1 = 3 Chukua 3+4+9+12+2.5 = 30.5

Yanga ina pointi 29 ikiwa 2024/25 Makundi (Klabu Bingwa) 1×5 = 5 2023/24 Robo (Klabu Bingwa) 3×4 = 12 2022/23 Mshindi 2(Shirikisho) 4×3 = 12 2021/22 Haikufuzu Makundi = 0 2020/21 Haikufuzu Makundi = 0 Chukua 0+0+12+12+5 = 29

Rejea kwenye aya ya kwanza huko juu nilisema Yanga imetengeneza pointi 5 huku Simba imetengeneza pointi 2.5 msimu huu kwa kufanikiwa kufuzu makundi, ukishafuzu makundi tapewa pointi za awali za kufuzu makundi, Yanga pointi 5 zimepatikana kwa kuchukua pointi 1 ya kufuzu makundi ya klabu bingwa zidisha na code ya msimu huu 5 (1×5=5) unapata pointi 5. Simb pointi 2.5 zinapatikana kwa kuchukua pointi 0.5 ya kufuzu makundi ya shirikisho zidisha na code ya msimu huu 5 (0.5×5= 2.5) unapata 2.5

Naomba tuelewe kuwa pointi za awali za kufuzu makundi ni sawa na timu uliyoishia nafasi ya nne kwenye kundi ila ukafanikiwa kumaliza nafasi ya tatu kwenye kundi au kufuzu robo fainali pointi zinaongezeka ila huwezi kupewa pointi zote za hatua hiyo wanajumlisha pointi ambazo bado mfano kufuzu robo klabu bingwa pointi 15 hawatajumlisha 15 zote watajumlisha 10 kwa sababu 5 ulipewa baada ya kufuzu makundi.

Yanga inaweza kuidizi Simba kwenye Club Ranking kivip? Twende pamoja iwapo timu zote zitafanikiwa kufuzu robo fainali ya klabu bingwa kwa Yanga na kombe la shirikisho kwa Simba zitakuwa na pointi zifuatazo.

Yanga kwa sasa ina pointi 29 ikifanikiwa kufuzu robo fainali ya klabu bingwa itakuwa imetengeneza pointi 15 (3×5) msimu huu chukua 29 toa 5 ambazo iliwekewa mwanzoni baada ya kufuzu makundi ya klabu bingwa zinabaki 24 jumlisha na 15 iwapo itafuzu robo (24+15 = 39) jumla Yanga inakuwa na pointi 39.

Simba kwa sasa ina pointi 30.5 ikifanikiwa kufuzu robo fainali ya kombe la shirikisho itakuwa imetengeneza pointi 10 (2×5) msimu huu chukua 30.5 toa 2.5 ambazo aliwekewa mwanzoni baada ya kufuzu makundi ya kombe la shirikisho zinabaki 28 jumlisha na 10 iwapo itafuzu robo (28+10=38) jumla Simba inakuwa na pointi 38

Je 38 na 39 ipi kubwa?
Ila iwapo timu zote Yanga na Simba zitafanikiwa kufuzu nusu fainali, Yanga klabu bingwa itakuwa na pointi 44 huku Simba kombe la shirikisho utakuwaa na pointi 43 iwapo Yanga itafuzu nusu na Simba ikaishia robo Yanga itakuwa na pointi 44, Simba itakuwa na pointi 38 na Iwapo Simba itafuzu nusu na Yanga ikaishia robo, Simba itakuwa na pointi 43 na Yanga itakuwa na pointi 39.
logoblog

Thanks for reading YANGA WAKIKAZA HAPA WATAMPOTEZA MAZIMA SIMBA CAF

Previous
« Prev Post

No comments:

Post a Comment