Thursday 10 October 2024

HESLB Majina Ya Waliopata Mkopo Awamu Ya Pili 2024/2025 Academic Year

  AjiraLeo Tanzania       Thursday 10 October 2024
WARNING
Beware of Job Scammers!
Please Never Pay Money To Get A Job!
HESLB Majina Ya Mkopo Awamu Ya Kwanza 2024/2025 Academic Year
HESLB
ORODHA YA PILI YA WANUFAIKA WA MKOPO HESLB 2024/2025 YATANGAZWA

💥MPYA: UNAFELI WAPI? INSTALL/UPDATE APP YETU. CLICK HERE!💥

💥UNASUBIRI NINI? FOLLOW US ON INSTAGRAM. CLICK HERE!💥

HESLB YATANGAZA ORODHA YA PILI WANUFAIKA 2024/2025

HESLB, Majina Ya Waliopata Mkopo Awamu Ya Pili 2024/2025 Academic Year, Majina Ya Waliopata Mkopo 2024/2025, Majina Ya Waliopata Mkopo Awamu Ya Pili 2024/2025, Majina Ya Waliopata Mkopo Awamu Ya Pili 2024, Waliopata Mkopo Awamu Ya Pili 2024/2025, Waliopata Mkopo Awamu Ya Pili 2024, Majina ya Mkopo Awamu Ya Pili 2024/2025, Wanuafaika wa Mkopo HESLB 2024/2025.

HESLB Majina Ya Mkopo Awamu Ya Pili 2024/2025 Academic Year

Wanafunzi wa shahada mwaka wa kwanza 30,311

Wanufaika 2,157 mikopo ya ‘Diploma’

Wanafunzi 588 kunufaika na ‘Samia Scholarship’

TZS 99.7 bilioni kutumika kuwagharimia mikopo, ruzuku TZS 2.9 bilioni

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) leo Jumatano (Oktoba 09, 2024) imetangaza awamu ya pili ya orodha ya wanafunzi wenye sifa waliopangiwa mikopo na ruzuku kwa ajili ya mwaka wa masomo 2024/2025.

Makundi ya walionufaika katika Awamu ya Pili

Orodha iliyotangazwa leo inajumuisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliodahiliwa katika vyuo mbalimbali vya elimu ya juu na vyuo vya kati waliopangiwa mikopo kwa ajili ya Shahada ya awali (30,311) yenye thamani ya TZS 93.7 bilioni. Orodha ya awamu ya pili inafanya idadi ya jumla ya wanafunzi 51,645 waliopangiwa mikopo katika awamu ya kwanza na awamu ya pili kwa ajili ya kugharimia masomo yao ya shahada ya awali ikiwa na thamani ya TZS 163.8 bilioni. Kati ya wanafunzi hao, wanafunzi wa kike ni 22,216 (sawa na 43%) na wa kiume 29,429 (sawa na 57%)

Awamu hii ya pii inajumuisha pia mikopo ya Stashahada (Diploma) kwa wanafunzi wapatao 2,157 yenye thamani ya TZS 5.6 bilioni. Wanafunzi wengine 45 ni wa shahada ya uzamili waliopangiwa mikopo yenye thamani ya TZS 205.6 milioni na wanufaika 16 wa Shahada ya Uzamivu waliopangiwa mikopo yenye thamani ya TZS 215.6 milioni.

Kuhusu kutangazwa kwa orodha ya Awamu ya Tatu

HESLB inaendelea kupokea taarifa za udahili kuwezesha kupanga mikopo na kutangaza Awamu ya tatu ya orodha ya wanafunzi waliopangiwa mikopo kwa mwaka 2024/2025 itakayotangazwa siku chache zijazo ili kuwawezesha wanafunzi waliopangiwa mikopo kuendelea na taratibu za kujisajii katika vyuo walikodahiliwa.
Read Also:

Samia Scholarship

Taarifa hii pia ina idadi ya wanafunzi 588 wa shahada ya awali watakaonufaika na fursa za ‘Samia Scholarships’ kwa mwaka huu 2024/2025, ambao wamepangiwa ruzuku yenye thamani ya TZS 2.9 bilioni. Wanafunzi hawa ni wenye ufaulu wa juu katika tahasusi za sayansi na waliodahiliwa katika vyuo mbalimbali kwenye fani za Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na hisabati na sayansi za Tiba.

Wito

HESLB inawakumbusha waombaji wa mikopo na ruzuku wenye sifa kwa mwaka 2024/2025 ambao bado hawajapangiwa mikopo au ruzuku, kuendelea kufuatilia taarifa za maombi yao kupitia ‘SIPA’ wakati taratibu za uchambuzi na upangaji wa mikopo na ruzuku zikiendelea.

Imetolewa na:
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
Jumatano, Oktoba 09, 2024.

KUCHEKI MAJINA HESLB, CLICK HERE!

logoblog

Thanks for reading HESLB Majina Ya Waliopata Mkopo Awamu Ya Pili 2024/2025 Academic Year

Previous
« Prev Post

No comments:

Post a Comment