Tuesday 9 July 2024

CV ya Boka Chadrak Beki Mpya Wa Yanga 2024/2025 Hii Hapa

  AjiraLeo Tanzania       Tuesday 9 July 2024
WARNING
Beware of Job Scammers!
Please Never Pay Money To Get A Job!

CV ya Boka Chadrak Beki Mpya Wa Yanga 2024/2025

Cv YA Boka Chadrak Beki Mpya Wa Yanga 2024/2025

Klabu ya Yanga SC imeendelea kuimarisha kikosi chake kwa kusajili mlinzi mahiri, Boka Chadrak, kutoka FC Saint Eloi Lupopo ya Kinshasa, Congo. Boka, ambaye ni mlinzi wa kushoto, anasifika kwa uwezo wake wa kushambulia na kujilinda kwa haraka, na atakuwa sehemu muhimu ya kikosi cha timu ya Wananchi Yanga sc kwa msimu wa 2024/2025.

CV Boka Chadrak Beki Mpya Wa Yanga 2024/2025

Maelezo Taarifa
Jina la Kuzaliwa Chadrack Issaka Boka
Tarehe ya Kuzaliwa/Umri Nov 20, 1999 (24)
Mahali pa Kuzaliwa Kinshasa, DR Congo
Uraia DR Congo
Nafasi Beki – Kushoto
Mguu wa Kutumia Kushoto
Klabu ya Sasa Yanga SC
Amejiunga Tarehe 8-Jul-24
Ametoka Klabu FC Saint Eloi Lupopo

Uwezo na Ujuzi wa Boka Chadrak

Boka Chadrak ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa cha kupandisha mashambulizi na kushuka haraka. Uwezo wake wa kuoverlap, yaani kupanda mbele kushambulia na kurudi haraka kujilinda, unamfanya kuwa chaguo bora kwa kocha Miguel Gamondi ambaye ni muumini wa mfumo wa 4-2-3-1. Mfumo huu unahitaji mabeki wenye uwezo wa kushambulia na kujilinda kwa kasi, kitu ambacho Boka anafanya kwa ufanisi mkubwa kutokana pumzi pamoja na spidi alionayo.
MUHIMU:

Mfumo wa 4-2-3-1 na Nafasi ya Boka Chadrak

Kocha Miguel Gamondi ametumia sana mfumo wa 4-2-3-1 katika msimu uliopita, na mara nyingi mfumo huu umekuwa ukitumika na timu zinazofanya pressing kwa kasi kama Yanga SC. Ingizo la Boka Chadrak linaongeza ufanisi wa mfumo huu kutokana na uwezo wake wa kuchezeshwa kama invited winger, ambapo atapanua uwanja na kuingia ndani kwa ajili ya kupiga pasi za hatari au krosi.

Katika mfumo huu, viungo washambuliaji watatu wanaocheza nyuma ya mshambuliaji wanategemea zaidi mabeki wa pembeni kama Boka na Kouasi Yao kupanua uwanja. Hii inafanya Boka kuwa na jukumu muhimu katika kuandaa mashambulizi na kutoa msaada kwa washambuliaji.

CHECK NAFASI MPYA ZA AJIRA NA FURSA. BOFYA HAPA!

logoblog

Thanks for reading CV ya Boka Chadrak Beki Mpya Wa Yanga 2024/2025 Hii Hapa

Previous
« Prev Post

No comments:

Post a Comment