Tuesday 9 July 2024

CV ya Ahoua Jean Charles Mchezaji Mpya Wa Simba SC 2024/2025

  AjiraLeo Tanzania       Tuesday 9 July 2024
WARNING
Beware of Job Scammers!
Please Never Pay Money To Get A Job!

CV ya Ahoua Jean Charles Mchezaji Mpya Wa Simba SC 2024/2025: Klabu ya Simba SC imethibitisha kukamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji Ahoua Jean Charles raia wa Ivory Coast 🇨🇮 kwa mkataba wa miaka miwili. Ahoua kinda fundi wa boli mtoto wa afu mbili mwenye umri wa miaka 22 ametokea Stella Club d’Adjamé ya nchini kwao Ivory Coast huku akiwa ndiye MVP wa msimu wa 2023/2024.

CV ya Ahoua Jean Charles Mchezaji Mpya Wa Simba SC 2024/2025

Katika msimu wa 2023/24, Ahoua ameibuka kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu nchini Ivory Coast (MVP) na klabu yake, huku akifunga mabao 12 na kutoa ‘assist’ tisa. Kiungo huyu mshambuliaji anasifika kwa kufunga mabao mengi nje ya box, kuchezesha timu, pamoja na kutengeneza nafasi kwa wenzie.

MUHIMU:

Mashabiki wengi wa simba wanategemea mambo makubwa kutoka kwa Ahoua kwa kushirikiana na nyota wengine ambao wameshasajiliwa pamoja na wale waliokuwepo kikosini. Kuelekea msimu wa Ligi 2024/25, Klabu ya Simba imekuja na utaratibu mpya kwenye usajili wa kuingiza wachezaji bora wenye uwezo na umri mdogo ili kujenga timu imara ya muda mrefu.

Ahoua anakuwa mchezaji wa nne kusajiliwa baada ya Lameck Lawi, Joshua Mutale, na Steven Mukwala. Usajili huu ni hatua muhimu kwa Simba SC, ikilenga kuimarisha kikosi chao kwa ajili ya michuano mbalimbali ndani na nje ya nchi. Wapenzi na mashabiki wa Simba SC wana matumaini makubwa kuona mchango wa Ahoua katika kufanikisha malengo ya klabu kwa msimu ujao.

CV ya Ahoua Jean Charles Mchezaji Mpya Wa Simba 2024/2025

Kipengele Maelezo
Tarehe ya kuzaliwa/Umri 10 Februari, 2002 (22)
Mahali pa kuzaliwa Zikisso, Cote d’Ivoire
Urefu 1.73 m
Uraia Cote d’Ivoire
Nafasi Kiungo – Kiungo mshambuliaji
Mguu wa kulia
Wakala wa mchezaji Jamaa
Klabu ya sasa Simba SC
Alijiunga 3 Julai, 2024
Alipotoka Stella Club d’Adjamé
Mkataba unaisha 2026
Nafasi kuu Kiungo mshambuliaji
Nafasi nyingine Winga wa kulia na winga wa kushoto

Safari ya Soka ya Ahoua Jean Charles

Ahoua Jean Charles ameanza safari yake ya soka la kulipwa kwa umahiri mkubwa, akionesha kiwango bora katika klabu mbalimbali nchini Cote d’Ivoire. Huu hapa ni muhtasari wa historia ya uhamisho wake:

Msimu Tarehe Klabu Aliyoondoka Klabu Aliyojiunga
20/21 1 Julai, 2020 LYS Sassandra Séwé Sports
22/23 1 Julai, 2022 Séwé Sports Stella Club
logoblog

Thanks for reading CV ya Ahoua Jean Charles Mchezaji Mpya Wa Simba SC 2024/2025

Previous
« Prev Post

No comments:

Post a Comment